JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

CHUO CHA TAIFA CHA HALI YA HEWA

NMTC Logo
Chuo kinakaribisha maombi kwa waombaji wenye sifa kusoma Cheti na Diploma katika Taaluma ya Hali ya Hewa yaani: Cheti cha awali (NTA Level 4), Cheti (NTA Level 5), Diploma (NTA Level 6) na Cheti cha awali NTA 4 na Cheti NTA 5 katika taaluma ya TEHAMA  kwa mwaka wa masomo 2025/2026. SIFA ZA KUJIUNGA (HALI YA HEWA) (a) CHETI CHA AWALI (Basic Technician Certificate (NTA Level 4) in Meteorology); Mwaka mmoja. Mwombaji awe amemaliza kidato cha nne (Form IV) na kufaulu walau masomo manne ikiwemo Fizikia na Hisabati na yasiusishe masomo ya dini. (b) CHETI (Technician Certificate (NTA Level 5) in Meteorology); Mwaka mmoja. Mwombaji awe na Cheti cha Awali cha Hali ya Hewa (Basic Technician Certificate (NTA level 4) in Meteorology) AU awe amemaliza kidato cha sita (Form VI PCM / PGM) na kufaulu masomo ya Fizikia na Hisabati katika kiwango cha ufaulu wa “Principal Pass” au zaidi kwa masomo yote mawili; au “Principal Pass” moja na “Subsidiary” moja miongoni mwa masomo hayo. (c) DIPLOMA (Ordinary Diploma (NTA Level 6) in Meteorology); Mwaka mmoja. Mwombaji awe na Cheti cha Hali ya Hewa (Technician Certificate (NTA level 5) in Meteorology) SIFA ZA KUJIUNGA (TEHAMA) (a) CHETI CHA AWALI (Basic Technician Certificate (NTA Level 4) in Information and Communication Technology); Mwaka mmoja. Mwombaji awe amemaliza kidato cha nne (Form IV) na kufaulu walau masomo manne ikiwemo Kingereza na Hisabati na yasihusishe masomo ya dini. AU Mwombaji awe na Cheti cha ufundi ngazi ya 3 (level 3) katika fani inayohusiana na teknolojia ya habari na mawasiliano na awe amemaliza kidato cha nne (Form IV) na kufaulu walau masomo manne ikiwemo Hisabati na yasiusishe masomo ya dini. (b) CHETI (Technician Certificate (NTA Level 5) in Information and Communication Technology); Mwaka mmoja. Awe amemaliza kidato cha sita na kufaulu  walau masomo mawili yasiyohusisha masomo ya dini kiwango cha ufaulu wa “Principal Pass”au zaidi , aidha awe na ufaulu wa "credit pass" katika Hisabati na kingereza katika masomo yake ya kidato cha nne Waombaji wote wenye sifa wanaweza kutuma maombi yao kwa kujaza fomu ya maombi. Kupata fomu ya maombi pakua hapa Barua au fomu zote za maombi zitumwe kwa: Mkuu wa Chuo, Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa, S. L. P 301, Kigoma. au kupitia barua pepe: nmtc@meteo.go.tz Kwa mawasiliano zaidi piga: +255 713883383 – Afisa Udahili Masomo yanatarajia kuanza mwezi Oktoba 2025 WMO Training Course on Radar Meteorology at the National Meteorological Training Centre (NMTC) of Tanzania Meteorological Authority to be held in Mwanza, United Republic of Tanzania from 26 to 30 August 2024. For more information click here  

Matangazo

NAFASI ZA KUJIUNGA NA MASOMO KWA NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA KATIKA MWAKA WA MASOMO 2025/2026
Chuo kinakaribisha maombi kwa waombaji wenye sifa kusoma Cheti na Diploma katika Taaluma ya Hali ya Hewa yaani: Cheti cha awali (NTA Level 4), Cheti (NTA Level 5), Diploma (NTA Level 6) na Cheti cha awali NTA 4 na Cheti NTA 5 katika taaluma ya TEHAMA  kwa mwaka wa masomo 2025/2026. SIFA ZA KUJIUNGA (HALI YA HEWA) (a) CHETI CHA AWALI (Basic Technician Certificate (NTA Level 4)...
2025-06-09 11:53:00
WMO TRAINING COURSE ON RADAR METEOROLOGY
WMO Training Course on Radar Meteorology at the National Meteorological Training Centre (NMTC) of Tanzania Meteorological Authority to be held in Mwanza, United Republic of Tanzania from 26 to 30 August 2024. For more information click here  
2024-06-25 11:35:56
Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania