Astashahada ya Hali ya Hewa
Astashahada ya Hali ya Hewa
Astashahada ya Hali ya Hewa (NTA LEVEL 5) ambayo inatambulika na Shirika la Hali ya Hewa Duniani kama ‘WMO-Meteorological Technician Mid-Level’. programu hii ni ya Mwaka mmoja yenye mihula miwili ikihusisha Jumla ya moduli kumi na mbili (12).
Muhitimu wa programu hii anaweza kufanya kazi ya uangazi wa hali ya hewa, aidha Muhitimu anatarajiwa kufanya kazi katika sekta mbalimbali kama vile Usafiri wa anga, Kilimo, Maji, Utalii, Ikolojia, Ulinzi na Usalama, Uvuvi, Viwanda, Ujenzi, Taasisi za Elimu na Utafiti,Usafiri wa Majini na nchi Kavu na Menejimenti ya Maafa.