MAHAFALI YA ISHIRINI NA MBILI (22) YA CHUO CHA TAIFA CHA HALI YA HEWA

19 Agosti, 2025, Kigoma:
Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa kilichopo chini ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kimeadhimisha mahafali ya ishirini na mbili (22) ya chuo hicho yaliyofanyika katika Viwanja “Chuo cha Taifa Cha Hali ya Hewa”.
Mgeni rasmi wa mahafali hayo alikuwa ni Dkt. Emannuel Mpeta ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, ambaye pia aliambatana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na Makamu Mwenyekiti wa jopo la wataalamu wa mabadiliko ya Tabia nchi (IPCC) Dkt. Ladislaus Chang`a. Kaimu Mkurugenzi Mkuu, pia aliambatana na Ndg. Brayson Kunyalanyala Mkurugenzi wa huduma saidizi, CPA Elizabeth Baraka Meneja huduma za fedha na Bi. Tunsume Mwamboneke Meneja mafunzo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania,
Katika mahafali hayo ya 22, Mkuu wa Chuo alimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu kwa jitihada zake za dhati katika kuendelea kukiwezesha Chuo na kufanikisha kuwezesha kuwa na wahitimu wa programu mpya ya technolojia ya habari “IT” ngazi ya Cheti cha awali kwa mara ya kwanza. Aidha, aliipongeza Bodi ya Chuo iliyo chini ya Dkt. Emmanuel Mpeta kwa Kuendelea kuishauri menejimenti ya Mamlaka ya Hali ya Hewa katika kutatua changamoto mbalimbali za Chuo.
Aidha, katika hotuba yake Kaimu Mkurugenzi mkuu Dkt. Lasdislaus Chang`a aliwapongeza wahitimu wote na kuwataka wafanye kazi kwa bidii ili kuweza kutatua changamoto zinazoikabili jamii kwa ujumla.
Pamoja na kuwatunuku wahitimu Hamsini na sita (56), kutoa vyeti vya pongezi kwa wahitimu waliofanya vizuri kitaaluma na cheti kwa mwanafunzi mwenye nidhamu, Mgeni rasmi Dkt. Emmanuel Mpeta alisema “Napenda kuchukua nafasi hii kushukuru Uongozi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Pamoja na uongozi wa Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa, Kigoma kwa kunipa heshima ya kuwa mgeni rasmi wa Mahafali ya 22 ya astashahada ya awali, Astashahada na Stashahada za Hali ya Hewa pamoja na astashahada ya awali ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa mwaka 2024/2025”
Katika hotuba yake pia alisema “Ili nchi yetu na dunia kwa ujumla ifanikiwe kuelekea maendeleo endelevu, taarifa sahihi za hali ya hewa kwa wakati muafaka zinahitajika kwa kiasi kikubwa”
Mwisho mgeni rasmi aliwaasa wahitimu na wageni waalikwa wote kutumia haki yao ya msingi ya
Kupiga kura katika uchaguzi mkuu.