Historia

Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa (NMTC) chini ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) kilianzishwa mnamo mwaka 1978 baada ya kuvunjika kwa iliyokua Jumuiya ya Afrika Mashariki. Lengo la kuanzishwa kwa chuo hiki ni kuwezesha Taifa kuongeza rasilimali watu katika taaluma ya Hali ya Hewa. Mnamo mwaka 1983 chuo kilihamishiwa katika Mkoa wa Kigoma, manispaa ya ujiji kutoka Dar es salaam kilipokuepo hapo awali.

Chuo kilikuwa kinatoa Mafunzo ya cheti kinachotambulika na Shirika la Hali ya Hewa duniani (WMO) daraja la tatu na la nne.Mnamo mwaka 2005 chuo kilianza kutoa Mafunzo ya cheti cha hali ya hewa daraja la pili(WMO Meteorological Technician, Senior Level).

Kwa sasa Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa(NMTC) kimesajiliwa na kinatambulika na Baraza la Taifa la vyuo vya Ufundi(NACTE). Kilisajiliwa rasmi na NACTE mwezi wa tatu mwaka 2014 kwa namba REG/EOS/025.Pia Chuo kinatambulika na Shirika la Hali ya Hewa Duniani(WMO).