Habari

Imewekwa: 03/05/2023

ZIARA YA MRATIBU WA MAENDELEO YA ELIMU NA MAFUNZO KUTOKA SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI

ZIARA YA MRATIBU WA MAENDELEO YA ELIMU NA MAFUNZO KUTOKA  SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI

Chuo cha hali ya Hewa kimetembelewa na Dkt. Paul Bugeac ambaye ni Mratibu wa Maendeleo ya Elimu na Mafunzo kutoka Shirika la hali ya hewa duniani “WMO”

Mratibu huyo ameambatana na Meneja wa Mafunzo na muwakilishi kutoka kitengo cha ushirikiano wa kikanda na kimataifa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, akiwa na lengo la kujadili masuala ya kielimu na mafunzo kwa ujumla na jinsi ambavyo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inaweza kushirikiana na wadau wengine wa Hali ya Hewa duniani. Majadiliano hayo yalihusisha wakufunzi wa Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa na kuongozwa na mkuu wa chuo Ndugu Peter Nicky Mlonganile.

Dkt Paul alizungumzia umuhimu wa kuendesha Kozi za muda mfupi na jinsi ambavyo Chuo kinaweza kujitangaza na kujulikana kimataifa kupitia “WMO Global Campus”

Aidha, alisisitiza kwenye utoaji wa mafunzo yenye kuzingatia umahiri “Compence based training” ili kukidhi mahitaji ya wadau wa huduma za hali ya hewa.

Mratibu huyo pia ameweza kutembelea “radar site” kuangalia maendeleo ya mradi wa usimikwaji wa radar Kigoma unaoendelea maeneo ya Nyamori