Wasifu

Card image cap
Mkuu wa Chuo
Bwana Peter Nicky Mlonganile

Bwana Peter Nicky Mlonganile ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa (NMTC) tangu mwaka 2016. Bwana Mlonganile aliajiriwa na “TMA” mwaka 2003 na alianzia ngazi ya “Meteorologist Trainee” ambapo alikua ni mhitimu wa shahada ya “Bachelor of Science with Education”. Awali bwana Peter Mlonganile alifanya kazi katika sehemu mbalimbali kabla ya kujiunga na “TMA” ikiwemo ni ualimu katika shule za sekondari. Shule za sekondari alizofundishani Mtwango katika mkoa wa Njombe, Kongwa katika mkoa wa Dodoma na Shule ya wasichana Iringa “Iringa Girls”ambapo alikua akifundisha masomo ya Fizikia na Hisabati.

Ari na nia ya kutumikia na kusaidia nchi yake hususani katika eneo la utoaji wa huduma za hali ya hewa kwa jamii ili kukabiliana na athari za hali mbaya ya hewa, ilimfanya Bwana Mlonganile ajiendeleze kielimu kwa kujiunga na masomo ya “Post graduate diploma in Meteorology” katika chuo kikuu cha Nairobi Kenya na kuhitimu mwaka 2014; pia alijiendeleza na kujiunga na masomo ya shahada ya uzamili (Msc. In Mathematical Modeling) katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam na kuhitimu mwaka 2012. Pia Bwana Mlonganile ameshiriki kozi fupiza kitaifa na kimataifa kwa muda tofauti tofauti ikiwemo Improving weather forecast in East Africa through WRF-4Dvar data assimilation technique” katika chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa kipindi cha mwaka mmoja 2003-2004,” Use of Eta Model as a tool for numerical weather prediction over Tanzania: Verificational analysis” katika chuo kikuu cha Nairobi mwaka 2004, “Dynamical Downscaling of the SRES A1B Greenhouse Gas Scenario for” Tanzania katika nchi ya Ujerumani katika kipindi cha Aprili na Junimwaka 2009.

Mafanikio na mchango wa Bwana Mlonganile katika fani ya hali ya hewa ni pamoja na utoaji wa elimu ya “TDCF” katika nchi za “SADC” na za Afrika Mashariki ikiwemo Malawi, Mozambique, Zimbabwe, Lesotho, Kenya, Rwanda, Botswana na Seychelles.

Bwana Mlonganile ameoa na ni baba wa watoto watano.