Karibu NMTC

Dkt. Ladislaus Chang'a

Kwa niaba ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), napenda kuwakaribisha katika Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa (NMTC), kilichopo chini ya Mamlaka ya Hali ya Hewa ambacho kinapatikana Mkoa wa Kigoma katika manispaa ya Kigoma-Ujiji.

Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa ni chuo pekee kinachotoa taaluma ya hali ya hewa nchini, lengo kuu ni kuwawezesha watanzania na wale wa nje ya nchi kupata mafunzo na ujuzi wa sayansi ya hali ya hewa kutoka kwa wakufunzi wenye uzoefu.

Kwa heshima na taadhima nawakaribisha wanafunzi pamoja na taasisi kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi kujiunga na chuo hiki ambacho kina mitaala bora inayokidhi kutoa mafunzo kwa wanafunzi kutoka ndani na nje ya nchi kwa kuzingatia viwango vya NACTE na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO).

Chuo kimejidhatiti katika kutoa wahihitimu wenye uwezo wa kufanya kazi katika mazingira mbalimbali, ikiwemo yale yanayotumia vifaa vya kisasa vya hali ya hewa.

Kwa mara nyingine, napenda kuwakaribisha katika Chuo cha Hali ya Hewa ili kupata mafunzo yenye ubora wa kimataifa.

Dkt. Ladislaus Chang'a

Kaimu Mkurugenzi Mkuu