MAHAFALI YA 21 CHUO CHA TAIFA CHA HALI YA HEWA

18 Desemba, 2024, Kigoma:
Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa kilichopo chini ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kimeadhimisha mahafali ya ishirini na moja (21) ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa “Joy in the Harvest- Kigoma”.
Mgeni rasmi wa mahafali hayo alikuwa ni Dkt. Emannuel Mpeta ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, ambaye pia aliambatana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na Makamu Mwenyekiti wa jopo la wataalamu wa mabadiliko ya Tabianchi (IPCC) Dkt. Ladislaus Chang`a. Kaimu Mkurugenzi Mkuu, pia aliambatana na Ndg. Brayson Kunyalanyala Mkurugenzi wa huduma saidizi, CPA Heleni Mwakifunda Meneja huduma za fedha na Bi. Tunsume Mwamboneke Meneja mafunzo Mamlaka ya Hali ya Hewa,
Katika mahafali hayo ya 21, Mkuu wa Chuo alimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu kwa jitihada zake za dhati katika kuendelea kukiwezesha Chuo na kufanikisha kuanzishwa kwa programu mpya ya technolojia ya habari “IT”. Aidha, aliipongeza Bodi ya Chuo iliyo chini ya Dkt. Emmanuel Mpeta kwa Kuendelea kuishauri menejimenti ya Mamlaka ya Hali ya Hewa katika kutatua changamoto za Chuo.
Aidha, katika hotuba yake Kaimu Mkurugenzi mkuu Dkt. Laslaus Chang`a aliwapongeza wahitimu wote na kuwataka wafanye kazi kwa bidii ili kuweza kutatua changamoto zinazoikabili jamii kwa ujumla.
Pamoja na kuwatunuku wahitimu 37 wa taaluma za Hali ya Hewa na kutoa vyeti vya pongezi kwa wahitimu waliofanya vizuri kitaaluma. Mgeni rasmi Dkt. Emmanuel Mpeta alisema “Napenda kuchukua nafasi hii kushukuru Uongozi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Pamoja na uongozi wa Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa, Kigoma kwa kunipa heshima ya kuwa mgeni rasmi wa Mahafali ya 21 ya astashahada ya awali, Astashahada na Stashahada za Hali ya Hewa kwa mwaka 2024”
Katika hotuba yake pia alisema “Ili nchi yetu na dunia kwa ujumla ifanikiwe kuelekea maendeleo endelevu, taarifa sahihi za hali ya hewa kwa wakati muafaka zinahitajika kwa kiasi kikubwa”