JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

CHUO CHA TAIFA CHA HALI YA HEWA

NMTC Logo
NAFASI ZA KUJIUNGA NA MASOMO KWA NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA KATIKA MWAKA WA MASOMO 2024/2025
25 Jun, 2024

Chuo kinakaribisha maombi kwa waombaji wenye sifa kusoma Cheti na Diploma katika Taaluma ya Hali ya Hewa yaani: Cheti cha awali (NTA Level 4), Cheti (NTA Level 5), Diploma (NTA Level 6) na Cheti cha awali katika taaluma ya Tehama (NTA 4) kwa mwaka wa masomo 2024/2025.

SIFA ZA KUJIUNGA (HALI YA HEWA)

(a) CHETI CHA AWALI (Basic Technician Certificate (NTA Level 4) in Meteorology); Mwaka mmoja.

Mwombaji awe amemaliza kidato cha nne (Form IV) na kufaulu walau masomo manne ikiwemo Fizikia na Hisabati na yasiusishe masomo ya dini.

(b) CHETI (Technician Certificate (NTA Level 5) in Meteorology); Mwaka mmoja.

Mwombaji awe na Cheti cha Awali cha Hali ya Hewa (Basic Technician Certificate (NTA level 4) in Meteorology) AU awe amemaliza kidato cha sita (Form VI PCM / PGM) na kufaulu masomo ya Fizikia na Hisabati katika kiwango cha ufaulu wa “Principal Pass” au zaidi kwa masomo yote mawili; au “Principal Pass” moja na “Subsidiary” moja miongoni mwa masomo hayo.

(c) DIPLOMA (Ordinary Diploma (NTA Level 6) in Meteorology); Mwaka mmoja.

Mwombaji awe na Cheti cha Hali ya Hewa (Technician Certificate (NTA level 5) in Meteorology)

SIFA ZA KUJIUNGA (TEHAMA)

CHETI CHA AWALI (Basic Technician Certificate (NTA Level 4) in Information Technology); Mwaka mmoja.

Mwombaji awe amemaliza kidato cha nne (Form IV) na kufaulu walau masomo manne ikiwemo Kingereza na Hisabati na yasihusishe masomo ya dini.

AU

Mwombaji awe na Cheti cha ufundi ngazi ya 3 (level 3) katika fani inayohusiana na teknolojia ya habari na mawasiliano na awe amemaliza kidato cha nne (Form IV) na kufaulu walau masomo manne ikiwemo Hisabati na yasiusishe masomo ya dini.

Waombaji wote wenye sifa wanaweza kutuma maombi yao kujaza fomu ya maombi. Kupata fomu ya maombi pakua hapa

Barua au fomu zote za maombi zitumwe kwa:

Mkuu wa Chuo,

Chuo cha Taifa Hali ya Hewa,

S. L. P 301,

Kigoma.

au kupitia barua pepe: nmtc@meteo.go.tz

Kwa mawasiliano zaidipiga: +255 653465699 – Afisa Udahili

Masomo yanatarajia kuanza mwezi Oktoba 2024

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania