Habari

Imewekwa: 07/09/2022

VULI 2022: MVUA ZA CHINI YA WASTANI HADI WASTANI ZINATARAJIWA KATIKA MAENEO MENGI YA NCHI

VULI 2022: MVUA ZA CHINI YA WASTANI HADI WASTANI ZINATARAJIWA KATIKA MAENEO MENGI YA NCHI

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi utabiri wa msimu wa mvua za Vuli 2022 kwa maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka. Akizungumza wakati wa mkutano na vyombo vya habari katika Makao Makuu ya TMA, Ubungo Plaza, Tarehe 2/9/2022, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Kijazi alisema maeneo ya nchi yanayopata misimu miwili ya mvua yanatarajiwa kupata mvua za chini ya wastani hadi wastani. Kusoma zaidi bofya hapa