Habari

Imewekwa: 25/05/2020

UFUNGUZI WA CHUO

UFUNGUZI WA CHUO

Uongozi wa Chuo Cha Taifa Cha Hali ya Hewa unapenda kuwatangazia wanafunzi wote kuwa chuo kitafunguliwa na masomo kuanza rasmi tarehe 01 Juni 2020. Wanafunzi wanaokaa Hosteli ya Chuo wataanza kuripoti kuanzia tarehe 29 Mei 2020.

Aidha mitihani iliyosalia ya “supplementary” itafanyika kuanzia tarehe 01 Juni 2020 hadi 03 Juni 2020.

Chuo kinawahimiza wanafunzi wote kuzingatia maelekezo yote ya Serikali na wataalam wa afya kuhusu udhibiti wa kuenea kwa ugonjwa wa Corona (COVID 19) kama uvaaji wa barakoa , unawaji wa mikono kwa maji tiririka na pia matumizi ya visafisha mikono muda wote ambao watakaokuwa maeneo ya Chuo na Hosteli.

Imetolewa na

MKUU WA CHUO

25 Mei 2020