Habari

Imewekwa: 07/07/2022

MAHAFALI YA 19 YA CHUO CHA TAIFA CHA HALI YA HEWA TAREHE 07/07/2022.

MAHAFALI YA 19 YA CHUO CHA TAIFA CHA HALI YA HEWA  TAREHE 07/07/2022.

Chuo cha Taifa Cha Hali ya Hewa kimefanya mahafali ya 19 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa "Joy in the harvest". Katika sherehe hizo za mahafali mgeni rasmi alikuwa ni Dkt.Makame Omary Makame ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Cha Taifa cha Hali ya hewa.

Katika hotuba yake mgeni rasmi aliipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa kuwezesha mafunzo katika chuo cha Hali ya Hewa.

“Natoa pongezi nyingi kwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kwa kuwezesha mafunzo haya kufanyika na leo tunashuhudia mahafali ya wahitimu waliobobea kwenye masuala ya Hali ya Hewa kwa ngazi ya NTA Level 4,NTA Level 5 na NTA Level 6”.Alisema Dkt. Makame.

Dkt. Makame pia alielezea umuhimu wa Hali ya Hewa katika maendeleo ya jamii na uchumi wa Taifa katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo,uvuvi,maji,uzalishaji Nishati,usafiri wa anga,majini na nchi kavu na kusema mafanikio ya shughuli hizi zote yanategemea sana taarifa za Hali ya Hewa.

Aidha Dkt.Makame alitoa rai kwa Wahitimu wote wakawe mabalozi wazuri katika kuelimisha jamii kuhusiana na umuhimu wa taarifa za Hali ya Hewa na kuzingatia tahadhari zitolewazo na Mamlaka Nchini ili kusaidia wanannchi kuepuka madhara yatokanayo na maafa.

Mwisho, mgeni rasmi aliwapongeza wahitimu wote,wakufunzi na wafanyakazi wote wa Chuo pamoja na meneja wa Uwanja wa ndege Kigoma kwa kazi nzuri ya kuwaandaa wahitimu kwa kuwapatia ujuzi wa taaluma ya Hali ya Hewa na kuwahimiza kushiriki katika Sensa kwa maendeleo ya Taifa.

“Napenda kumalizia kwa kusema Mamlaka ya Hali ya Hewa inawaomba tujiandae kuhesabiwa siku ya jumanne tarehe 23 Agosti ,2022”