Habari

Imewekwa: 08/04/2022

NAFASI ZA KUJIUNGA NA MASOMO KWA NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA KATIKA MWAKA WA MASOMO 2022/2023

NAFASI ZA KUJIUNGA NA MASOMO KWA NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA KATIKA MWAKA WA MASOMO 2022/2023

Chuo Cha Taifa Cha Hali ya Hewa kinakaribisha maombi ya kujiunga na kozi za hali ya Hewa kwa mwaka wa masomo 2022/2023.

Waombaji wote wenye sifa wanaweza kutuma maombi yao kwa kuandika barua au kujaza fomu ya maombi inayopatikana kwa kiunganishi https://www.nmtc.ac.tz/publications/application-forms na kuituma kwa Mkuu wa Chuo.

Maombi yote yaambatanishwe na kivuli cha cheti cha taaluma, cheti cha kuzaliwa na hati halisi ya malipo (Paying Slip) kiasi cha Tshs. 10,000 ilipwe kupitia Mfumo wa malipo wa serikali baada ya kupata namba ya kumbukumbu ya malipo kwa kupiga namba 0755395960 au 0746544380.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 15/09/2022 saa 9:30 alasiri.

Masomo kwa mwaka wa masomo 2022/2023 yataanza mwezi Oktoba 2022.

Barua au fomu zote za maombi zitumwe kwa:

Mkuu wa Chuo,

Chuo cha Taifa Hali ya Hewa,

S. L. P 301,

Kigoma-Tanzania.

Au kwa kutumia Barua pepe : nmtc@meteo.go.tz

Kwa mawasiliano zaidi piga: +255 653 465 699 – Afisa Udahili