Habari

Imewekwa: 04/08/2020

NAFASI ZA KUJIUNGA NA MASOMO KWA NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA KATIKA MWAKA WA MASOMO 2020/2021

NAFASI ZA KUJIUNGA NA MASOMO KWA NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA KATIKA MWAKA WA MASOMO 2020/2021

Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa ni chuo cha serikali chini ya Mamlaka ya Hali ya Hewa, kina uzoefu wa zaidi ya miaka arobaini (40) katika kufundisha wataalamu wa Hali ya Hewa.

Chuo kimepewa ithibati kamili na Baraza la Taifa la Mafunzo ya Ufundi (NACTE) kutoa mafunzo katika ngazi ya Cheti na Diploma (NTA level 4, 5 & 6) katika mfumo wa umahili (CBET).

Chuo kinakaribisha maombi kwa waombaji wenye sifa kusoma Cheti na Diploma katika Taaluma ya Hali ya Hewa kwa mwaka wa masomo 2020/2021.

SIFA ZA KUJIUNGA

a) CHETI CHA AWALI (Basic Technician Certificate in Meteorology, NTA Level 4); Mwaka mmoja.

Mwombaji awe amemaliza kidato cha nne (Form IV) na kufaulu walau masomo manne ikiwemo Fizikia na Hisabati na yasiwe ya dini.

b) CHETI (Technician Certificate in Meteorology, NTA Level 5); Mwaka mmoja.

Mwombaji awe amemaliza kidato cha sita (Form VI PCM / PGM) na kufaulu masomo ya Fizikia na Hisabati katika kiwango cha ufaulu wa “Principal Pass” na zaidi kwa masomo yote mawili; au “Principal Pass” moja na “Subsidiary” moja miongoni mwa masomo hayo.

AU Mwenye cheti cha awali (Basic Technician Certificate in Meteorology, NTA Level 4).

c) DIPLOMA (Ordinary Diploma in Meteorology, NTA Level 6); Mwaka mmoja.

Mwombaji awe na Cheti cha Hali ya Hewa (Technician Certificate in Meteorology, NTA level 5)

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30/08/2020 saa 9:30 alasiri.

Masomo kwa mwaka wa masomo 2020/2021 yataanza tarehe 15 Novemba 2020.